Meneja
huyo wa Manchester United alicheza kama kipa katika mechi hiyo
Game4Grenfell kati ya timu mbili za watu mashuhuri na wacheza soka wa
zamani.
Kikosi chake kilishindwa kwa mabao 5-3 kwa njia ya penalti, ambapo bingwa wa olimpiki Sir Mo Farah alifunga bao.
Takriban watu 80 walifariki wakati jengo la Grenfell lilishika moto magharibi mwa London tarehe 14 mwezi Juni.
Watu mashuhuri walishiriki mechi hiyo wakiwemo mcheza filamu Damian Lewis na Olly Murs.
Fedha kutoka kwa tikiti za mechi hiyo zilienda kwa mfuko wa wale walioathiriwa na janga la moto.
Wakati wa mapumziko waimbaji Rita Ora, Emeli Sande na Marcus Mumford walitumbuiza umati kwa nyimbo zao.
0 comments:
Post a Comment