Nyota wa
Taifa Stars, Saimon Msuva ameonyesha kwamba ni hatari katika kufunga
baada ya kukimbizana na staa wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda,
Emanuel Okwi.
Msuva aliifungia Stars mabao yote mawili
wakati ikiilaza Botswana 2-0 jana Jumamosi hivyo kufikisha idadi ya
mabao matatu katika mechi mbili za mwisho alizocheza.
Kabla
ya kujiunga na Stars, Msuva alitoka kuifungia timu yake ya Difaa El
Jadida ya Morocco bao moja katika ushindi wa 3-1 dhidi ya CR Khemis
Zemamra.
Hata hivyo Msuva anakimbizwa na Okwi ambaye
amefunga mabao matano katika mechi mbili za mwisho alizocheza. Okwi
aliifungia Simba mabao manne katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu
Shooting kabla ya kuifungia Uganda bao pekee la ushindi dhidi ya Mirsi
juzi Ijumaa.
0 comments:
Post a Comment