Haikuwa siku nzuri kwa Antonio Conte na mbinu za Pep Gurdiola
zilimpoteza kabisa, ilikuwa mbaya kwa Chelsea kwani ndio mchezo wa
kwanza kwa Chelsea kupiga mashuti machache.
Chelsea hawajawahi kupiga mashuti yaliyolenga bao chini ya 5 tangu
Conte ajiunge nao, lakini hii leo wamepiga mashuti manne tu huku kuanzia
dakika ya 26 hadi mpira unaisha walipiga mashuti mawili tu.
Manchester
City walipata bao lao la kwanza na la pekee kupitia kwa Kelvin De
Bruyne na kuwafanya sasa kuwa wamecheza michezo minne mfululizo
wakishinda bila kuruhusu bao katika Epl.
Kule nchini Ufaransa Kylian Mbappe alifunga moja ya bao katika
ushindi wa bao 6 kwa 2 dhidi ya Bordeaux na kumfanya kinda huyo kuhusika
katika mabao 29 ya ligi ya Ligue 1 msimu huu akifunga 14 na kuasisst 5.
0 comments:
Post a Comment