STRAIKA
wa Simba Mghana Nicholas Gyan aliyesajiliwa msimu huu akitokea klabu
ya Ebusua Dwarfs ya Ligi Kuu Ghana juzi alianza makeke kwa kutupia bao
na kulichanganya benchi la ufundi la klabu hiyo.
Benchi
hilo linakuna kichwa kuhakikisha kuwa Mghana huyo na Emmanuel Okwi
wanacheza pamoja ili kuzalisha mabao mengi, jambo litakalowaacha nyota
wengine nje.
Gyan alifunga bao la tatu wakati Simba
ikiifunga Hard Rock ya Pemba mabao 5-0 kwenye mechi ya kirafiki
iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Gyan
aliliambia Mwanaspoti kuwa kiu yake ni kuona anafunga kila mechi na
anashukuru aliweza kufanya hivyo juzi na ataendelea kufanya hivyo hata
katika Ligi Kuu Bara.
“Baada ya kufanya vizuri katika
ligi ya nyumbani Ghana, sasa nimekuja Simba ili kuendeleza kasi yangu ya
ufungaji, Simba haitajuta kunisajili,” alisema.
Hata
hivyo, Kocha Msaidizi wa Simba Jackson Mayanja alisema kwa namna Gyan
alivyoonyesha uwezo, ni lazima wapangue safu ya ushambuliaji na kuunda
kombinesheni mpya kwa nia ya kumpa nafasi sambamba na Okwi.
“Ni
straika aliyeonyesha uwezo wa hali ya juu na ametupa kazi ya
kurekebisha safu ya ushambuliaji ili kutengeneza kombinesheni
itakayoleta manufaa Simba,” alisema.
Kocha Mayanja
alisema Gyan ni straika ambaye walikuwa wakimsaka kwa muda mrefu na
kupatikana kwake ni wazi mashabiki wa klabu hiyo watasuuzika nyoyo zao.
Mpaka anaondoka Ghana, Gyan alikuwa wa tatu kwa kufumania nyavu kwa kufunga mabao 11.
0 comments:
Post a Comment