Kocha wa Yanga, George Lwandamina amerejea nchini akitokea kwao Zambia alipokuwa katika msiba wa baba yake na kuongoza mazoezi ya kikosi chake kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Lwandamina baada ya kufika katika kikosi hicho kilichokuwa kinajifua katika uwanja wa Uhuru,alianza kwa kuzungumza na benchi la ufundi akiongozwa na meneja wa timu hiyo Saleh Hafidh.
Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru, kikijiandaa na mechi dhidi ya Njombe Mji.
Yanga imeanza msimu huu wa ligi kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Lipuli iliyopanda daraja msimu huu.
0 comments:
Post a Comment