Thursday, 14 September 2017

MANENO YA WEMA BAADA YA MANJI KUACHIWA HURU

Baada ya mfanyabiashara mashuhuri nchini, Yusuf Manji kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu jijini Dar, Staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu ameonyesha kufurahishwa na kitendo hicho kutokana na ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa Instagram.
Siku za nyuma Wema alikuwa akiposti picha za Manji na kuandika ujumbe wa kusikitishwa na kumuonea huruma mfanyabiashara huyo, lakini saa chache baada ya kusambaa kwa taarifa za kuachiwa, ameposti tena picha ya Manji na kuandika maneno yafuatayo:

“Alhamdullilah”

Manji ameachiwa huru leo Septemba 14, baada ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuiambia mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive