Wednesday, 13 September 2017

JULIO AIPIGA DONGO SIMBA

 
Kocha mkongwe anayefundisha Dodoma FC ya Daraja la Kwanza, Jamhuri Kihwelo “Julio” ameipiga dongo timu ya Simba juu ya hali inayoendelea katika timu hiyo kuhusu Kocha Mkuu Joseph Omog na viongozi huku akilinganisha na hali katika timu yake ya sasa.
Julio amefunguka kuwa, timu nyingi za Kitanzania viongozi wanapenda kusajili wachezaji wanaowataka wao na sio makocha hivyo kusababisha timu nyingi kutokufanya vizuri.
“Mfano Simba viongozi wameleta wachezaji wanaowataka wao na sifikiri kama kocha aliwahitaji wote wale, lakini sasa wameanza kumuandama kocha kwa jinsi mwelekeo unavyoenda na wanataka kuwa juu zaidi ya kocha,” alisema.
“Na hii kwangu naona ni changamoto sababu timu nimeikuta tayari wachezaji wamesajiliwa na timu ina sapoti kubwa sana kwa viongozi jambo linalofanya kuwepo na presha kubwa sana,” aliongeza.
Akiongea kuhusu changamoto nyingine, Julio anasema, Kwake Ligi Daraja la Kwanza anaijua vizuri sana kutokana na uzoefu alionao hivyo amejiandaa vizuri kuhakikisha msimu ujao timu yake inashiriki ligi kuu.
“Jumapili tunaanza kibarua chetu na Pamba ya Mwanza baada ya hapo tutaenda Musoma na kurudi tena ambapo kwa sasa ninachokifanya ni kukiunganisha kikosi ili kiwe fiti kwa ajili ya mapambano hayo ambayo si rahisi kama watu wanavyofikiria,” alisisitiza Julio.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive