Chadema imetangaza kuanzisha kampeni maalumu kuchangisha fedha kwa
ajili ya kumgharimia mbunge wake, Tundu Lissu anayeendelea kupata
matibabu mjini Nairobi huku matibabu yake yakigharimu Sh 10 milioni kwa
siku.
Kutokana na ukubwa wa gharama hizo chama hicho tayari kimeziomba
jumuiya za kimataifa ikiwamo Ujerumani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya(EU)
kuangalia kama inaweza kusaidia matibabu ya mwanasiasa huyo.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari amesema leo Ijumaa kuwa pamoja na gharama za kumtibu Lissu kuwa kubwa lakini chama kitaendelea kumpigania ili kuokoa maisha yake.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari amesema leo Ijumaa kuwa pamoja na gharama za kumtibu Lissu kuwa kubwa lakini chama kitaendelea kumpigania ili kuokoa maisha yake.
“Unajua chama tumepoteza watu wengi sana, kama vile Ben Saanani, Dk
Slaa ( Willbroad) lakini tuna mahaba makubwa na ndugu yetu Lissu hivyo
tunaendelea kupigania maisha yake. Gharama anazotumiwa kutibiwa ni kubwa
mno maana kwa siku inagharimu kiasi cha Sh10 milioni sasa sisi peke
yetu hatuwezi ndiyo maana tumeamua kuomba msaada toka kwa rafiki zetu,”
amesema.
Amesema chama kimeunda kamati maalumu ambayo inaratibu michango ya
Lissu na moja ya eneo ambalo wamewasilisha maombi yao ni kwa Serikali ya
Ujerumani na Umoja wa Ulaya.
“Siwezi kusema hadi sasa nini tumejibiwa ila ninachojua kamati inaendelea kufuatilia… unajua wale Wajerumani ni ndugu zetu maana chama cha CDU ni marafiki zetu na tumewaandikia,” amesema.
“Siwezi kusema hadi sasa nini tumejibiwa ila ninachojua kamati inaendelea kufuatilia… unajua wale Wajerumani ni ndugu zetu maana chama cha CDU ni marafiki zetu na tumewaandikia,” amesema.
Chama cha Christian Democratic Party (CDU) kinachoongozwa na Angela
Merkel kwa sasa kipo kwenye kampeni za kumchangua Kansela katika
uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu. Vyama hivi, Chadema na CDU
vimekuwa na uhusiano wa kisiasa kwa muda mrefu na mara kwa mara viongozi
wake wamekuwa wakitembeleana.
“Chadema inaamini kuwa kutokana na kufikwa na tatizo hilo huenda
kikapata msaada kutoka miongoni mwa vyama rafiki.” Pia, alidokeza kuwepo
uwezekano wa kuiandikia Uingereza katika juhudi zake za kuomba
usaidizi.
Profesa Safari amesema chama kimejaribu kukusanya michango kutoka kwa
kanda zake pamoja na wananchi wengi lakini kadri siku zinavyoenda
gharama zimekuwa zikiongezeka hivyo wameamua kupiga hodi pia katika
jumuiya za kimataifa.
“Wananchi wetu ni maskini na Serikali hadi sasa haijataka kuchangia
gharama zozote hivyo lazima tuendelee kutafuta njia nyingine za kumwokoa
ndugu yetu,”amesema.
0 comments:
Post a Comment