MMOJA wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi uliopita, Edward Lowassa, leo amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, anayetibiwa jijini Nairobi baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma wiki iliyopita.
Ujumbe wa Lowassa ambao ameuweka kwenye mtandao wa Twitter unasema kwa Kiingereza kwamba: Earlier
today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of
TLS and dear friend (Mapema leo nilikwenda Hospitali ya Nairobi kumwona
Mbunge na Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) ambaye ni
rafiki yangu mkubwa.)
Lissu alishambuliwa na
kujeruhiwa vibaya kwa risasi na watu ambao hawajulikani alipokuwa
anarejea nyumbani kwake mchana baada ya kikao bungeni ambapo alikimbizwa
Hospitali ya Dodoma na hatimaye Nairobi kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment