WABUNGE wa CUF wameonekana kuvurugana Bungeni Mjini Dodoma leo Jumatatu, Septemba 11, kutokana na mgogoro unaoendelea katika chama hicho baada ya wabunge wanaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma kuwa mwenyekiti wao bungeni.
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson
alitangaza kuwa Spika, Job Ndugai amepokea barua kutoka kwa Katibu wa
CUF, Magdalena Sakaya kuhusu safu hiyo ya uongozi.
Baada ya tangazo hilo, Mbunge wa
Malindi, Ally Salehe aliomba mwongozo wa Spika akitaka kujua ni nani
anaamua kuhusu uongozi wa wabunge bungeni kwa sababu wao wameshafanya
uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kuwa mwenyekiti
wao baada ya kufukuzwa kwa wabunge wanane. Pia, amehoji inawezekanaje kuwa na viongozi wawili bila wa kwanza kufutwa?
Akijibu mwongozo huo, Dk Tulia amesema
Spika amepokea taarifa ya viongozi hao lakini hajapokea taarifa ya
uchaguzi wa upande wa akina Ally Salehe ambao unamuunga mkono Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. Amesema watakapopeleka taarifa yao ndipo Spika ataamua.
0 comments:
Post a Comment