Monday, 11 September 2017

DAKTARI AFUNGUKA HAYA KUHUSU KAMUSOKO

Baada ya kushindwa kumaliza mchezo dhidi ya Njombe Mji, kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko amerejea kwenye mazoezi baada ya kupata ruhusa ya daktari.


Kamusoko alianza mchezo huo vizuri kwenye Uwanja wa Sabasaba ambapo timu yake ilipata ushindi wa bao 1-0, lakini alishindwa kumaliza dakika 90 ambapo alitoka kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Rafael Daudi.

Haikujulikana kwa haraka juu ya kilichosababisha akashindwa kuendelea kucheza licha ya kutoka uwanjani akitembea mwenyewe bila msaada wa mtu yeyote.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa Kamusoko alipata majeraha madogo lakini alirejea uwanjani leo Jumatatu na kuendelea na mazoezi kama kawaida baada ya kuruhusiwa na daktari wa timu aliyemfanyia uchunguzi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive