KIUNGO wa Simba, Myarwanda, Haruna Niyonzima, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo, akidai licha ya matokeo ya sare waliyoyatoa dhidi ya Mbao, anaamini timu hiyo itatwaa ubingwa mwishoni mwa msimu.
Simba ambayo ina pointi nane katika
msimamo wa ligi, imetoa sare michezo miwili na kushinda michezo miwili
kati ya michezo minne iliyocheza.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima amesema kuwa, kikosi chao kipo vizuri na wanaamini watafanikiwa kutwaa ubingwa licha ya upinzani mkubwa wanaokumbana nao.
“Kikosi cha Simba kwa ujumla kipo
vizuri kwani hata mabao tuliyofungwa na Mbao yalikuwa ya kushtukiza,
tulimiliki mpira kwa asilimia 90 ya mchezo na kilichotokea ni bahati
tu ambayo haikuwa yetu.
“Kwa ubora wa kikosi chetu kilivyo, nina imani ya kuweza kutwaa ubingwa msimu huu, kikubwa zaidi ni kuweza kujituma uwanjani,” alisema Niyonzima.
0 comments:
Post a Comment