Monday, 25 September 2017

TSHISHIMBI AIKOROGA YANGA

BAADA ya Yanga kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC kutoka Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa juzi Jumamosi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mchezaji wake mpya Papy Tshishimbi amepata kadi ya tatu ya njano na atakosa mechi ijayo kati ya timu yake dhidi ya Mtibwa.
Katika mechi hiyo, mshambuliaji mpya kutoka kwa mahasimu wao Simba , Ibrahim Ajib, ndiye aliyefungia bao dakika ya 35 baada ya kazi nzuri ya beki wa kati, Kelvin Yondani.
Beki wa kulia, Juma Abdul Mnyamani alimuanzishia kona fupi Yondani, ambaye alitoa krosi safi iliyounganishwa nyavuni na Ajib kwa staili ya kukunjuka.
Tshishimbi alionyeshwa kadi za njano mara ya kwanza katika mechi na Lipuli na Njombe Mji ambapo kadi ya tatu alionyeshwa na refarii Jeonisya Rukyaa kwenye mchezo dhidi ya Ndanda FC.
Hata hivyo Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema kumkosa Tshishimbi katika mechi ijayo ni pengo lakini wako watakaoliziba.
Kocha huyo aliongeza kwamba, benchi la ufundi litaanza kulifanyia kazi mapema pengo hilo watakapokutana na Mtibwa Sugar, Jumamosi ijayo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive