BEKI kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema kuwa licha ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi
kufunga mabao sita hadi sasa, lakini ana kibarua kigumu mbele yake
kutokana na upinzani atakaokutana nao kutoka kwa washambuliaji wa Yanga,
akiwemo Amissi Tambwe.
Okwi ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufumania nyavu kwa kuwa na mabao sita hadi sasa.
Lakini Tambwe ambaye anaanza mazoezi leo Jumatatu, akiwa uwanjani kufunga huwa ni jadi yake, hatua ambayo inampa matumaini Cannavaro kuwa mshambuliaji huyo ataweza kumfikia Okwi na kuleta ushindani.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Cannavaro
amesema kuwa, mabao sita ya Okwi kwa sasa siyo kigezo cha mshambuliaji
huyo kuweza kutwaa ufungaji bora msimu huu na kudai kuwa atakutana na
upinzani mkali kutoka kwa washambuliaji wa Yanga akiwemo Tambwe mara
baada ya kurejea.
“Ni vigumu kumhakikishia kuwa Okwi
anaweza kuwa mfungaji bora katika kipindi hiki kwani tunaamini muda upo
na kwa upande wetu kuna Tambwe ambaye bado hajarejea, tunaamini atafanya
vizuri na kuleta ushindani kwenye mbio za ufungaji bora.
“Pia kuna wachezaji kama Chirwa
(Obrey), Ngoma (Donald) na Ajibu (Ibrahimu), wanao uwezo wa kufunga
vizuri na hata kuwania ufungaji bora, hivyo ligi bado na tunaamini
watafanya vyema,” alisema Cannavaro.
0 comments:
Post a Comment