STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema hakuweza kufanya vizuri
katika mchezo dhidi ya Mbao FC, kwani mabeki wa wapinzani wao hao
walimkamia kupita kiasi.
Okwi hakuweza kufurukuta dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu
Bara uliochezwa juzi Alhamisi kwani alitulizwa kwa kuchezewa rafu mara
12.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao
iliilazimisha Simba sare ya mabao 2-2 na kuwa timu ya kwanza kutikisa
nyavu za Wekundu wa Msimbazi msimu huu.
Okwi, mwenye mabao sita katika ligi kuu akiwa kinara wa ufungaji,
alishindwa kufunga kutokana na mabeki wa Mbao kuwa makini wakiongozwa na
Boniface Maganga na Yusuph Mgeta.
0 comments:
Post a Comment