Aliyekuwa mchezaji wa Chelsea, Diego Costa |
Diego Costa ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Atletico Madrid, amebainisha kuwa anafuraha sana kurejea nyumbani Hispania.
"Atletico ni nyumbani kwangu na sasa nimewasili," alisema Costa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amewasili nchini Hispania kupata matibabu baada ya kutangazwa siku ya Alhamisi kuwa klabu yake ya zamani imemsajili tena kutoka Chelsea kwa ada iliyoaminika kuwa ni £ 58m.
Costa alijiunga na Chelsea kutoka Atletico mwaka 2014 na wameshinda mataji mawili katika misimu mitatu, huku akicheza mechi 120 na kufunga mabao 59.
0 comments:
Post a Comment