Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, ameamua kuondoka katika klabu hiyo huku Real Madrid, Manchester City na Paris Saint-Germain zikipambana kumsajili (L'Equipe)
Barcelona tayari wamewasiliana na Monaco kuhusu Kylian Mbappe. (Le10Sport)
Ligi ya Uhispania haitokubali kupokea malipo ya kutengua kifungu cha uhamisho cha Neymar kutoka PSG kwa sababu ya mzozo wa malipo ya uzalendo kati ya Neymar na Barca na pia wasiwasi kuhusu PSG kukiuka kanuni za fedha za UEFA. (Sport)
UEFA itaitaka PSG kujieleza jinsi inavyopanga kupata fedha za usajili wa Neymar. (Daily Telegraph)
Barcelona hawatojaribu kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoinne Griezmann, 26, licha ya Neymar kuonekana kuwa anaondoka. (AS)
Barcelona wataziba pengo la Neymar kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele, 20, anayechezea Borussia Dortmund. (Marca)
Borussia Dortmund wamekataa dau la Arsenal la kumtaka Ousmane Dembele, 20. (Mundo Deportivo)
Wakala wa zamani wa Neymar Wagner Ribeiro amesema "PSG watalipa kitita cha kutengua kifungu cha usajili" wa mchezaji huyo wa Brazil na kuwa "Neymar atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wiki hii". (Marca)
Barcelona watatumia fedha za mauzo ya Neymar kwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, na Philippe Coutinho wa Liverpool. (Daily Mail)
Manchester United wapo tayari kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza kiungo chipukizi Scott McTominay, 20. (Daily Record)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema atakuwa "mwenye furaha" iwapo timu yake itaweza kusajili mchezaji mwingine tena. (Daily Express)
Jose Mourinho amesema mshambuliaji Anthony Martial, 21, haondoki Manchester United licha ya kuhusishwa na kuhamia Inter Milan. (Daily Star)
Meneja wa Man Utd Jose Mourinho angependa kusajili wachezaji wengine watatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hata hivyo United inaarifiwa wamekata tamaa ya kumsajili winga wa Inter Milan, Ivan Perisic. (Daily Express)
Meneja wa Tottenham anataka kumfanya kipa Paulo Gazzaniga, 25, kuwa usajili wake wa kwanza kwa kutoa pauni milioni 2 kwa Southampton. (Sun)
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simione ameiambia bodi ya klabu yake kuwa lazima wamsajili Diego Costa, 28, ambaye Chelsea wanasema anauzwa kwa pauni milioni 50. (Evening Standard)
Chelsea hawana haraka ya kumuuza Diego Costa, na wamedhamiria kushikilia bei ya pauni milioni 50. (Daily Star)
Chelsea wanatazamia kumsajili kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, 27, badala ya Renato Sanches, 19 wa Bayern Munich. (Mediaset)
Uhamisho wa pauni milioni 50 wa kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, kutoka Swansea kwenda Everton unatarajiwa kukamilika siku chache zijazo. (Guardian)
Beki wa Southampton anayenyatiwa na Liverpool Virgil van Dijk, 26, anakaribia kulazimisha uhamisho wake. (daily Mirror)Kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, huenda akakataa kusaini mkataba mpya na timu yake
Kiungo anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, huenda akakataa kusaini mkataba mpya RB Leipzig. (Bild)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
0 comments:
Post a Comment