Thursday, 3 August 2017

KIONGOZI WA UPINZANI APIGWA FAINI YA DOLA 5000

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amepigwa faini ya dola za kimarekani 5000 kwa kuandaa tukio lililopigwa marufuku na kuitisha wafuasi wake kujitokeza barabarani mapema mwezi Julai.
Ameshitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria ya kujipigia kampeni ya kupata kura.
Wafuasi wake wengine wawili nao wamepigwa faini kama hiyo.
Bwana Navalny ambaye amekuwa maarufu kwa kumkosoa Rais Putin amekusudia kugombea urais wa nchi hiyo katika uchaguzi ujao.
Lakini tume ya uchaguzi imesema hana sifa za kugombea kwa sababu alipatikana na hatia ya ufisadi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive