Jo'burg, Afrika Kusini. Mabingwa wa Kombe la FA, Simba imelazimisha sare ya bao 1-1 na Bidvest Wits katika mchezo wake wa pili wa kirafiki uliofanyika leo Afrika Kusini.
Katika mchezo bao pekee la Simba lilifungwa na beki mpya wa timu hiyo Erasto Nyoni katika dakika 32.
Matokeo hayo ni faraja kwa Simba inayojiandaa na mchezo wa Ngao wa Jamii dhidi ya Yanga baada ya kupokea kichapo katika mechi ya kwanza kwa bao 1-0 kutoka kwa Orlando Pirates.
Kikosi kilichoanza Simba ni. Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, Salim Mbonde, Method Mwanjali, James Kotei, Jamal Mnyate, Mdhamiru Yassin, John Bocco, Emmanuel Okwi, Mohamed Ibrahim.
0 comments:
Post a Comment