Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi.
Kuelekea mchezo wao wa Agosti 23, mwaka huu, tambo za upinzani baina
ya Simba na Yanga zimeendelea kuwa kubwa ambapo sasa timu hizo zote zipo
visiwani Zanzibar.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana katika mchezo huo wa
kuukaribisha msimu wa 2017/18 ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Kumekuwa na presha kubwa kuelekea mchezo huo kwa kuwa pande zote
zinaamini vikosi vyao vipo sawa, Yanga wapo Pemba wakati Simba wapo
Unguja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika amesema kikosi chao
kipo Pemba kwa ajili ya kuendeleza maandalizi ya msimu huo mpya, lakini
kuhusu Simba wao hawawafikirii kabisa.
Upande wa Mratibu wa Simba, Abbas Suleiman amesema
kikosi chao
kimeshatua Unguja kwa ajili ya kujiandaa na
msimu mpya na kuhusu Yanga,
hilo ni suala la mwalimu
anaweza kuzungumza zaidi lakini maandalizi yapo
vizuri
kwa upande wake.
Upande wa mashabiki wa timu hizo wamekuwa wakitishiana mitandaoni na
kila upande ukiona wenyewe upo vizuri na unaweza kufanya vizuri katika
mchezo huo ubaina ya timu zao.
0 comments:
Post a Comment