Juuko Murshid akiwa na Hans Pope.
KLABU ya Simba
imeendelea kuimarika zaidi baada ya beki wake Mganda, Juuko Murshid
kuungana na wenzake tayari kwa maandalizi ya mechi ya Ngao ya Jamii
dhidi ya Yanga.
Hiyo ni habari njema kwa kocha wa Simba
na mashabiki kutokana na uwezo na mchango wa Mganda huyo aliounyesha
katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.
Mwishoni mwa msimu Juuko alihusishwa na
kutaka kuondoka Simba na kutimkia Afrika Kusini kujiunga na Orlando
Pirates ambayo kwa sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Uganda, Milutin
Sredojevic ‘Micho’.
Mratibu wa Simba, Abbas Ali alisema
walikuwa na lengo la kumuuza Juuko kwa Orlando, lakini klabu hiyo
haikuwa na nia ya dhati kwani tangu beki alipofikia Afrika Kusini
hajawahi hata kufanya mazoezi na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini
humo.
Abbas alisema jina la Juuko
lilipendekezwa nakocha Micho aliyekuwa naye katika timu ya Taifa ya
Uganda, lakini mabosi wa Orlando hawakuwa na lengo la kusajili beki kwa
sasa.
“Juuko mkataba wake unamalizika
katikati ya msimu huu, lakini Micho alipopata kazi katika timu hiyo ya
Orlando alipendekeza jina lake ili asajiliwe, lakini mabosi wa timu hiyo
walitaka afanye kwanza majaribio na kama watalizika naye ndio wamsajili
katika kikosi chao,” alisema.
“Tangu alipofika nchini humu
hakufanikiwa kufanya mazoezi na timu hiyo hata siku moja, na ndio maana
tumemwambia arudi nchini ikiwa kujiunga na timu yake kwa ajili ya
maandalizi ya msimu mpya wa ligi na mashindano mingine na kama kweli
wanamuhitaji watamfuata tena,” alisema Abbas.
0 comments:
Post a Comment