Mjumbe
wa zamani wa kamati ya mashindano ya Yanga, Athumani Kihamia
amesikitishwa na kitendo cha klabu hiyo kutomsajili kiungo mshambuliaji
Mrisho Ngassa msimu huu.
Kihamia aliyejitoa kwenye
kamati ya mashindano ya klabu hiyo kwa madai ya kubanwa na majukumu ya
ukurugenzi wa jiji la Arusha, alisema kumuacha Ngassa katika kikosi chao
ni sawa na kuitupa bahati iliyojileta wenyewe
“Naheshimu
uamuzi ya kamati ilikuwa na kazi kubwa ya kufanya usajili, lakini kwa
maoni yangu niseme tu kumuacha mchezaji kama Ngassa aliyejileta mwenyewe
si sawa kwani angeweza kuitumikia klabu kwa gharama tuitakayo sisi si
kama wachezaji wengine waliokuwa wanatamka dau lao wenyewe.”
“Kiwango
alichonacho Ngassa ni sawa na Emmanuel Okwi (Simba) ambapo
wangesumbuana katika nafasi hiyo, hivyo uongozi ufanye utaratibu
mwingine wa kurudisha mchezaji huyo hata katika dirisha dogo kwani
kusema kuwa mwalimu hamhitaji ni hoja dhaifu kwani mwalimu huwa
analetewa mchezaji na kushawishiwa juu ya uwezo wake na kufanyiwa
majaribio na kukubalika au kukataliwa,” alisema Kihamia.
0 comments:
Post a Comment