Saturday 19 August 2017

SIMBA KUFANYA MABADILIKO JUMAPILI




 Kamati ya kuratibu mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Simba, imeeleza kukoshwa na mwitikio wa wanachama wake visiwani Zanzibar ambao wameunga mkono mchakato huo katika mkutano maalum iliyofanyika juzi.
Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa klabu ya Kikwajuni, uliandaliwa maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya mabadiliko wanachama wa Simba kabla ya mkutano mkuu wa kujadili suala hilo, utakaofanyika Jumapili jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu mchakato wa mabadiliko, Mulamu Nghambi aliliambia gazeti hili kuwa wanachama wa Simba, visiwani Zanzibar wameunga mkono mabadiliko ya uendeshaji wa timu hiyo kwenda mfumo wa hisa jambo ambalo linatoa ishara njema kuelekea mkutano mkuu.
"Kimsingi kote tulikopita kutoa elimu ya mabadiliko, Wanasimba wameonyesha kuunga mkono na kutoa maoni yao ambayo yamelenga kuboresha zaidi mabadiliko hayo kwa faida ya klabu yao.
Hapa Zanzibar mkutano wetu ulikuwa na wanachama 60 ambao wamewawakilisha wenzao na wote kwa kauli moja wameunga mkono huku tukifikia maazimio ya kila mmoja wao kwenda kuwaelimisha wenzake watatu, ili elimu hii iweze kusambaa kwa kila mmoja," alisema Nghambi.
Nghambi ambaye katika mkutano huo aliongozana na mjumbe wa kamati ya mashindano, Hassan Hassanoo na katibu mkuu wa zamani wa Simba, Mwina Kaduguda alisema kuwa suala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji haliepukiki kwa soka la Tanzania.
"Wanachama na mashabiki wa Simba wanatambua kuwa uendeshaji wa timu unagharama kubwa na ndio maana kwa wingi wao wameamua kuunga mkono hiki kinachofanyika," aliongeza Nghambi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive