Saturday 19 August 2017

KAGAME AWA MBOGO KWA MAREKANI


Rais Paul Kagame wa Rwanda jana ameapishwa kuongoza muhula wa tatu wa miaka saba ambapo ameyashutumu mataifa ya Magharibi kwa kuingilia siasa za ndani za taifa hilo.


Akihutubia maelfu ya wananchi na viongozi kadhaa wa Afrika waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rais Kagame amesema, kila jaribio lililofanywa la kupenyeza chuki limeshindwa na badala yake limewaunganisha zaidi Wanyarwanda.

Kuapishwa kwa Rais Kagame kunafuatia ushindi mkubwa alioupata baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 4 mwaka huu baada ya kushinda kwa asilimia 98.7% ambapo aliwashinda wapinzani wake Frank Habineza na Phillipe Mpayimana.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive