Rais
Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wakagana na Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
baada ya
kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa
Kanisa, katika Kanisa
Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo
Agosti 13, 2017.
Rais Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wakitakiana amani na watawa wakati wa
Ibada ya Misa hiyo.
Rais Magufuli akiwapungia mkono waumini baada ya kushiriki Ibada ya Misa.
Rais
Magufuli akipiga picha ya kumbukumbu na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu
Katoliki la
Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Padre
Vicent na baadhi ya
wanafunzi shule ya Sekondari ya St. Joseph baada ya
kushiriki Ibada ya Misa hiyo.
…Wakijumuika na waumini wengine kushiriki Ibada ya Misa hiyo.
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa takatifu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na
Mkewe, Mama Janeth Magufuli leo wameungana na waumini wengine kushiriki
Ibada ya Misa Takatifu, Dominika ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika
Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment