Aliyekuwa mgombea wa Nasa, Raila Odinga amewataka wananchi wa Kenya wanaomuunga mkono kutokwenda kazini siku ya kesho mpaka pale atakapotoa msimamo kuhusu kile anachoita wizi wa kura wakati wa uchaguzi.
Akizungumza na wafausi wake waliyojitokeza kwa wingi eneo la Kibera, nchini humo Odinga alisema kuwa siku ya Jumanne ndiyo atatoa msimamo wake.
Odinga aliwakilisha muungano wa Nasa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8 mwaka huu nchini Kenya lakini alishindwa kufurukuta baada ya Kenyatta kutetea kiti chake kwa kupata ushindi wa asilimia 64.
Odinga aliwaeleza wafuasi wake kuwa walitambua fika kuwa uchaguzi huo ungegubikwa na wizi wa kura na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
"Tulitabiri wangeiba kura na hicho ndicho kilichotokea. Hatuja maliza bado. Hatuta kata tamaa. Subiri hatua inayofuata nitatoa msimamo Jumanne."
"Ni wazi kuwa mamlaka husika zimeshindwa kuchukua hatua stahiki na badala yake wanaua watu. kura zimeibiwa hakuna cha kuficha hapo."
"Ila ninachoweza kuwaambia kwa sasa kesho msiende kazini," Alisema Odinga.
Wakazi wa Kibera walifurika kwa wingi kumsikiliza Odinga ambaye aliongea kwa mara ya kwanza tangu Kenyatta atangazwe kuwa mshindi wa kiti cha urais nchini humo.
0 comments:
Post a Comment