Pamoja
kuvuliwa uanachama na kusimamishwa katika nafasi ya Mkuu wa Baraza la
Wazee la Simba, Hamisi Kilomoni, ameonekana kushangazwa na taarifa hizo.
Mzee
Kilomoni amesema hana taarifa zozote kuhuhusiana na suala hilo ambalo
limefikiwa na wanachama wa Simba baada ya yeye kufungua kesi mahakamani
akipinga mkutano.
Mkongwe
huyo wa zamani wa Simba ambaye amekuwa akisigana na baadhi ya
wanachama, amesema anayeondolewa kwenye udhamini anapaswa kuwa kuwa
mgonjwa au mtu aliyehama zaidi ya mara moja jijini Dar es Salaam.
“Kweli sina taarifa lakini kuna taratibu za kufanya na si kama mnavyosema,” alisema.
Maana yake, mzee Kilomoni anaamini anaendelea kuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini.
Wanachama baada ya kumsimamisha mzee Kilomoni uanachama, nafasi yake ameteuliwa kuishika Adam Mgoyi.
0 comments:
Post a Comment