Monday 14 August 2017

ABDI BANDA ATESWA NA UGONJWA WA JINI KABULA

Abdi Banda,
ALIYEKUWA beki wa kati na kiungo wa Simba, Abdi Banda ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Moroka Swallows FC ya nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ amefunguka juu ya kuteswa na ugonjwa wa matatizo ya afya ya akili unaomkabili mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye aliwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu akiwa 
Sauz, Banda ambaye alidumu kwenye uhusiano na 
Kabula kwa muda mrefu alisema kuwa, anaumizwa 
mno na hali iliyompata zilipendwa wake huyo na kibaya 
zaidi yupo mbali naye, hivyo amekuwa akitumia watu 
wake wa karibu kumsaidia.

“Nilipokea taarifa za Jini Kabula kwa masikitiko makubwa, japokuwa sijajua chanzo cha tatizo lake ni nini, ninamuombea kwa Mungu apone haraka, nipo mbali ila nawasiliana na watu wangu wa karibu kumsaidia, nimeachana naye miaka miwili iliyopita lakini hawezi kuwa adui yangu, kwani hakuna aijue kesho,” alisema Banda huku Kabula akiwa bado hajapona na tatizo hilo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive