KIUNGO mpya wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima alitua nchini jana alfajiri akitokea kwao Rwanda tayari kwa kujiunga na
kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya maandalizi yake ya msimu ujao.
Hata hivyo, mara baada ya kutua nchini
viongozi wa Simba walilazimika kutumia mbinu za kimafia kumtoa katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya kubaini
kuwepo kwa mashabiki wa Yanga ambayo ilikuwa ni timu yake ya zamani.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya
Simba zimedai kuwa viongozi wa klabu hiyo waliofika uwanjani hapo
kumpokea, walibaini uwepo wa mashabiki hao na nia yao kubwa ilikuwa
kumfanyia fujo kwa kile ambacho kinadaiwa ni kukasirishwa na kitendo cha
kuhama kwenye timu yao na kwenda kwa watani wa jadi.
Kiongozi mmoja wa Simba ameliambia
gazeti hili kuwa walilazimika kuwasiliana na uongozi wa uwanja huo wa
ndege na kuwaeleza juu ya mkakati uliokuwa umepangwa kabla ya Niyonzima
kutoka ndani ya eneo la ukaguzi.
“Ilitubidi tumpitishie VIP, tuliomba
kwenye mamlaka za uwanja, wakaturuhusu, ilivyokuwa hivyo tukampitisha
huko kisha akaingia kwenye gari na tukaondoka naye, tukawaacha mashabiki
hao wa Yanga uwanjani hapo.
“Niyonzima alitua nchini na ndege ya
saa tisa alfajiri ya leo (jana) na tukaenda kumficha sehemu kabla ya
kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu
ujao wa ligi kuu,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Katika hatua nyingine, mshambuliaji wa
Simba raia wa Ghana, Nicolas Gyan naye aliyetegemewa kuwasili nchini
jana usiku ili kumalizia masuala ya usajili wake na Simba na kuna
uwezekano mkubwa akawa mmoja wa wachezaji watakaotambulishwa katika
Simba Day, kesho Jumanne.
0 comments:
Post a Comment