Mshambuliaji Nicolas Agyei leo ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya Simba.
Agyei ametambulishwa makao makuu ya klabu ya Simba baada ya kuwasili nchini leo usiku.
Raia huyo wa Ghana amekuwa ndiye mchezaji wa mwisho kujiunga wakati wa usajili.
Msemaji
wa Simba, Haji Manara ndiye aliyemtambulisha Agyei mbele ya baadhi ya
waandishi wa habari na baadhi ya wanachama wa Simba waliokuwa klabuni
hapo.
Pamoja
na Mghana huyo, wengine waliotambulishwa klabu hapo ni Haruna
Niyonzima, Emmanuel Okwi na wenyeji wawili, Method Mwanjale na Mohamed
Hussein Zimbwe.
0 comments:
Post a Comment