KIKOSI cha Simba kilirejea nchini juzi Jumamosi, kikitokea Afrika Kusini kilipokuwa kimepiga kambi kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2017/18, pia Kombe la Shirikisho Afrika.
Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba ambaye
ni raia wa Cameroon, Joseph Omog amemmwagia sifa za pekee mshambuliaji
wake mpya, Mganda, Emmanuel Okwi kwa kusema kuwa wamelamba dume, kwani
mchezaji huyo ni mashine uwanjani.
Akizungumza na Championi Jumatatu muda
mfupi tu baada ya kutua nchini, Omog alisema katika muda mfupi ambao
amekaa na Okwi katikia kikosi chake amegundua ana mambo mengi ambayo ni
tofauti kabisa na wachezaji wengine.
“Nashukuru Mungu tumerejea nchini
salama lakini pia kambi yetu ilikuwa ni nzuri sana na imetujenga vilivyo
kwa ajili ya msimu ujao na imeniwezesha kuwajua vizuri baadhi ya
wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni.
“Hata hivyo, nimevutiwa sana na Okwi,
kwani katika muda mfupi niliokaa naye kambini nimeweza kugundua mambo
mengi kutoka kwake ambayo ni tofauti kabisa na wachezaji wengine.
“Anajua majukumu yake anapokuwa
uwanjani, pia nje ya uwanja anajua afanye nini, hakika atakuwa msaada
mkubwa kwetu safari hii katika harakati zetu za kuwania ubingwa wa ligi
kuu ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la
Shirikisho Afrika,” alisema Omog na kuongeza:
“Kwa yeyote anayetaka kuthibitisha haya
ninayoyasema aje uwanjani siku ya Jumanne (kesho) tutakapopambana na
Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.”
0 comments:
Post a Comment