Kiungo
wa Simba, raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima ameweka wazi kuwa yeye ndiye
aliyemuomba kiungo mkongwe wa timu hiyo, Mwinyi Kazimoto amuachie jezi
namba nane aliyokuwa akiitumia msimu uliopita.
Niyonzima
amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga baada
ya mkataba wake kumalizika Julai 21, mwaka huu huku akigomea kusaini
timu yake ya zamani kutokana na kushindwana katika dau la usajili.
Kazimoto
amekuwa akitumia jezi namba nane tangu msimu uliopita lakini ameamua
kubadilisha na kuchukua namba 24 iliyokuwa ikitumiwa na Abdi Banda
aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini.
Niyonzima
amesema aliamua kumuomba jezi hiyo kwa kuwa tangu aanze kucheza soka
hajawahi kuvaa jezi yenye namba tofauti na hiyo jambo ambalo
linamuongezea bahati uwanjani.
“Kwangu
limekuwa ni tukio zuri kwa sababu kwanza kabisa Kazimoto namkubali kwa
kuwa ni mchezaji mzuri na mkubwa ambaye namuheshimu, kilichotokea ni
kwamba mimi mwenyewe nimemuomba na ameridhia kunipa jezi namba nane bila
ya kinyongo chochote.
“Kiukweli
ni kitu cha kumshukuru maana sikutarajia na nimemuahidi kwamba
nitamtafutia zawadi kwa sababu amenifanya nijisikie kucheza kwa amani
nikiwa ndani ya jezi namba nane maana tangu nianze kucheza mpira ndiyo
nimekuwa nikiivaa sijawahi kubadilisha namba,” alisema Niyonzima.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment