Kiungo
mkabaji wa Yanga kutoka DRC Congo, Papy Kabamba Tshishimbi anatarajiwa
kuwasili nchini leo Ijumaa kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.
Tshishimbi
hivi karibuni alitua nchini na kusaini mkataba wa miaka miwili ya
kuichezea timu hiyo kabla ya kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya kumaliza
matatizo ya kifamilia.
Awali,
kiungo huyo alishindwa kujiunga na Yanga kutokana na mkataba wake
kutomalizika katika kikosi cha Mbabane Swallows cha Swaziland.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema Tshishimbi
alitakiwa ajiunge na timu tangu wiki hii ilipoanza lakini hati yake ya
kusafiria (pasipoti) ndiyo ilikwamisha.
Aliongeza
kuwa, mara baada ya kutua nchini, kiungo huyo atakuwepo kwenye kikosi
kitakachoivaa Ruvu Shooting, kesho Jumamosi katika mechi ya kirafiki
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment