RUVU Shooting ya mkoani hapa, imesema
kikosi cha Simba kilichocheza na Rayon Sports ya Rwanda, Jumanne wiki
hii, hakina uwezo wa kuwafunga katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu
Bara Agosti 26, mwaka huu.
Katika Tamasha la Simba Day, Simba
iliifunga Rayon bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa
Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kama kuna mashabiki
wanakiona kikosi cha Simba ni kizuri, basi wamepotea kwani wao wanakiona
cha kawaida kisichoweza kuwasumbua.
Bwire ametamba kuwa wataishushia kipigo
kikali Simba watakapokutana kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu
itakayoanza Agosti 26, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment