Mshambuliaji
wa Yanga, Ibrahim Ajibu ataanza kuonekana akicheza tofauti na
ilivyokuwa Simba hasa katika wakati wa ushambulizi, pia kukaba.
Kocha George Lwandamina ameyasoma mapungufu ya Ajibu wakati akiwa Simba na taratibu amekuwa akiyafanyia kazi mapungufu hayo.
“Unajua
Ajibu alikuwa hakabi, lakini pia uchezaji wake licha ya kuwa na kipaji,
kocha aliona haukuwa ule wa malengo sana,” kilieleza chanzo ndani ya
Yanga.
“Utaona
kama vile anakaa na mpira muda mrefu bila sababu au kucheza na jukwaa.
Lakini kocha amemueleza kuwa ni lazima kufanya kazi kwa malengo kwa kuwa
dakika 90 ni chache sana lazima kuzitumia vizuri.”
Kweli mara kadhaa, Lwandamina ameonekana kufanya mazoezi na Ajibu akimsisitiza masuala kadhaa akionyesha amepania kumrekebisha.
0 comments:
Post a Comment