KATIKA kuiimarisha safu yao ya ulinzi, Yanga imemshusha nchini beki Mnigeria, Eisa Mfowoshe aliyemaliza mkataba wa kuichezea Klabu ya Itihad ya Oman.
Ujio wa beki huyo unakamilisha idadi ya wachezaji watatu waliokuwepo
kwenye majaribio ya timu hiyo wengine ni beki Mnigeria, Henry Okoh na
kiungo Fernando Bongyang na Mfowoshe.
Kati ya wachezaji hao mmoja pekee ndiye anatakiwa asajiliwe ili
akamilishe idadi ya wachezaji saba wa kimataifa kati ya sita ambao
tayari wamesajiliwa na Yanga. Championi Ijumaa
lilikuwepo kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam na kumshuhudia beki huyo akionyesha uzoefu wa
kupambana na washambuliaji wenye uwezo wa juu.
Katika mazoezi hayo, beki huyo mwenye umbile kubwa alionekana
akifanya program zote kwa makini huku akionyesha uhodari wake wa kupiga
pasi zilizonyooka ndefu na fupi kwa wenzake. Wakati mazoezi hayo
yakiendelea, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina alimpangia washambuliaji wawili, Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwa ajili ya kumpima.
Mnigeria huyo alionyesha uhodari wa kuwadhibiti
huku akitumia vema umbile lake kubwa kuokoa mipira ya juu kwa vichwa na
kupanga mabeki wenzake aliocheza nao akiwemo Kelvin Yondani kama vile
wameshacheza pamoja muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment