Monday, 7 August 2017

MWANARIADHA ALPHONCE SIMBU ANG'ARA LONDON



Mwanariadha Alphonce Simbu ameshinda medali ya shaba katika mbio ndefu za Marathon akimaliza nafasi ya tatu katika Mashindano ya Dunia ya Riadha London, Uingereza.
 Simbu alikimbia kwa saa 2:09:51 na kumaliza kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Mkenya, Geoffrey Kirui aliyemaliza kwenye nafasi ya kwanza akikimbia kwa saa 2:08:27 na Muethiopia, Tamirat Tola aliyemaliza wa pili akikimbia kwa saa 2:09:49.
Ushindi huo wa Simbu ni neema kwa Tanzania ambayo tangu 2005 ilipochukua medali kwenye mbio hizo huko Finland, haijawahi kushinda medali yoyote ya dunia hadi leo Jumapili Simbu kushinda Shaba.
Medali hiyo ya Simbu ilianza kuonekana mapema wakiwa wamekimbia umbali wa kilomita 21 (Nusu Marathon).
Kwa ushindi huo sasa Simbu ataondoka na kitita cha Dola 20,000 huku bingwa akizawadiwa Dola 60,000 na mshindi wa pili ataondoka na Dola 30,000.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive