Kiungo huyo aliyeichezea Mbao msimu uliopita, amefungiwa mwaka mmoja kutokana na kubainika kusaini timu mbili tofauti.
Kamati
ya Katika Sheria na Hadhi za wachezaji inayoongozwa na Richard
Sinamtwa, inegundua na kubaini Buswita amesaini mkataba na klabu mbili
tofauti katika msimu mmoja wa 2017/2018" ilisema taarifa na TFF
Taarifa
hiyo ilisema Kamati imebaini kwamba mchezaji huyo aliyechezea Mbao FC
ya Mwanza msimu uliopita, amevunja Kanuni ya 66 ya Ligi Kuu ambayo
inaelekeza adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja hivyo mchezaji huyo
amefungiwa kucheza mpira wa miguu kwa mwaka mmoja.
Pia
kamati hiyo imebaini upungufu katika uwasilishaji wa majina ya wachezaji
wa msimu wa 2017/18 kwa timu zote hivyo kuziagiza klabu zote kuleta
majina matatu ya wachezaji wasiopungua 18 na wasiozidi 30 wa kikosi cha
timu ya vijana (U20).
Klabu pia zimeagizwa kuanisha
wachezaji wa zamani na wapya na klabu wanazotoka kwa timu zote mbili za
wakubwa na vijana huku zikizingatia matakwa ya kanuni kwa kila mchezaji
ili aweze kupatiwa leseni.
Matakwa hayo ambayo
yamesisitizwa ni kila mchezaji kujaziwa fomu ya utimamu wa mwili,
kuwasilisha nakala tatu za mikataba ya wachezaji TFF, Uthibitisho wa
kukatiwa Bima, Barua ya Uhamisho kutoka timu ambayo ametoka pia
wachezaji wa kigeni kuwa na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na
kulipiwa Ada ya ushiriki ya msimu Sh. 2,000,000.
Wakati huo TFf imetangaza kuwa msimu ujao wa 2018/2019 Ligi Kuu Bara itapandisha idadi ya timu kutoka 16 ilivyo sasa hadi 20.
Kamati ya Utendaji ya TFF imefikia uamuzi huo juzi Jumanne katika kikao chake na sasa i inafanya marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Kamati ya Utendaji ya TFF imefikia uamuzi huo juzi Jumanne katika kikao chake na sasa i inafanya marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Kwa
marekebisho hayo, timu zitakazoshuka daraja msimu ujao kutoka Ligi Kuu
Bara zitakuwa mbili huku sita zikipanda daraja kutoka Ligi Daraja la
Kwanza.
Hiyo ina maana msimu huu timu mbili zitapanda kutoka katika kila kundi katika ligi daraja la kwanza.
Katika
Ligi daraja la kwanza, kundi A lina timu za African Lyon, Ashanti
United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za
Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya
Morogoro.
Kundi B lina Coastal Union ya Tanga; JKT
Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya
Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za
Dar es Salaam.
Wakati kundi C lina timu za Alliance
School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora,
Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga
na JKT Oljoro ya Arusha.
0 comments:
Post a Comment