KIba na Dimpoz.
Mitandaoni bhana kuna mambo! Waswahili wanasema fumbo mfumbie mjinga mwerevu
atalifumbua, kuanzia jana kwenye mitandao ya kijamii, kuna mafumbo
yanayoendelea ambayo baadhi ya mashabiki wameshayafumbua.
CHANZO NI NINI?
Kwa mujibu wa mashabiki wa muziki wanadai kwamba
chanzo kilianzia kwenye wimbo wa rapa Fid Q, unaoitwa Fresh, ambapo
ndani ya wimbo huo kuna mistari aliyoimba Diamond ya kumkashifu Kiba.
“Kunifananisha na Cinderela kwangu haiwezi kuwa fresh, Simba toka mbuga ya Tandale, naona Swala wanafosi tuwe saresare, si walitaka viti, nimewapa hadi kitanda wakalale” Hiyo ndiyo mistari inayomlenga Kiba.
Baada ya kuisikia ngoma hiyo, Kiba akapita kwenye akaunti yake ya Twitter na kujibu mapigo kwa staili ya mafumbo

MARA DIMPOZ NAYE KAHUSISHWA
Saa chache baada ya Posti ya Kiba, upande wa pili ukajibu
mashambulizi kwa kuachia audio yenye Verse 1 kwa kupitia beat ya wimbo
ule ule wa Fresh, ambapo ndani yake kamhusisha Kiba na Ommy Dimpoz.
KICHAA CHAMPANDA DIMPOZ
Dimpoz baada ya kuusikia wimbo huo, akaamua kuliamsha dude, ambalo
ndiyo linazizima mpaka sasa, huku mashabiki wakiwa na shauku ya kutaka
kujua upande wa pili utafanya nini.
0 comments:
Post a Comment