Baada ya ushindi murua waliopata klabu ya Simba hakika umedhihirisha maneno ya Kocha wa klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi, mkameroni Joseph Omog, aliyozungumza kabla ya mtanange huo.
ikiwemo na kuonesha uhodari wa wachezaji waliosajili msimu huu ambao ni maarufu na wenye uzoefu mkubwa kuliko timu nyingine za Ligi
Kuu Bara msimu huu.
Mastaa hao hatari iliosajili ni pamoja na Mganda Emmanuel Okwi ambaye ni
kipenzi cha mashabiki wa Msimbazi, John Bocco, Shomari Kapombe, Ally
Shomary, Aishi Manula na Said Mohammed ‘Nduda’.
ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo kocha wa klabu hiyo alizungumza mambo ikiwemo juu ya kile atakachowafanya wapinzani wake.
ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo kocha wa klabu hiyo alizungumza mambo ikiwemo juu ya kile atakachowafanya wapinzani wake.
“Kiujumla
usajili tulioufanya ni mzuri na viongozi wamefanikiwa kuniletea aina ya
wachezaji ninaowahitaji ili timu iweze kufanya vizuri msimu
unaotarajiwa kuanza hivi karibuni,” anasema kocha wa timu hiyo Mcameroon
Joseph Omog.
“Nimepata kundi kubwa la wachezaji
wazoefu, waliopevuka na wenye kiwango kizuri, ambao bila shaka watakuwa
na mchango mkubwa kwa timu katika mashindano mbalimbali ambayo
tutashiriki msimu ujao.
“Matarajio yetu ni kufanya
vizuri ambako si kwa namna nyingine bali kutwaa ubingwa kwenye kila
mashindano ambayo tutashiriki. Kiu ya mashabiki na kila mmoja ni kutaka
kuona timu inapata mafanikio ya kuchukua kombe na si vinginevyo. Msimu
uliopita tulifanikiwa kuchukua Kombe la FA tu lakini hatukufanikiwa
kubeba lile la Ligi Kuu.
“Kwa ubora wa kikosi cha Simba
hivi sasa, kipaumbele cha kwanza ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ambao
hatujafanikiwa kuuchukua kwa kipindi kirefu, pia tumepanga kutetea
ubingwa wa Kombe la FA sambamba na kufanya vizuri kwenye mashindano ya
kimataifa.
“Kambi zote mbili (Afrika Kusini na Unguja)
zimekuwa na mafanikio kwetu kwa sababu utulivu uliokuwepo umewasaidia
wachezaji kuelekeza akili zaidi kwenye programu za mazoezi na kuwa sawa
kisaikolojia, jambo ambalo litakuwa na faida kwa timu.
“Kupitia
kambi hizo tumepata nafasi ya kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza
msimu uliopita, hivyo naamini tutaingia kwenye ligi tukiwa tayari
kuikabili vita iliyo mbele yetu.
“Ligi itakuwa ngumu
kwa sababu nimesikia timu nyingi zikifanya usajili mzuri na kuanza
maandalizi mapema. Na ugumu huo hasa utakuwa kwetu kwa sababu timu
nyingi zimekuwa zikikamia sana pindi zinapokutana na Simba na ukiongeza
na huu usajili tulioufanya, tutakuwa na vita kubwa.”
Yanga na Kimataifa
Akiwazungumzia wapinzani wake wakubwa hao, Omog anasema:
“Yanga
ni timu nzuri ambayo kikosi chake hakijafanyiwa mabadiliko makubwa,
hivyo naamini watakuwa tishio. “Nimekuwa nikifuatilia mechi zao, kikubwa
kinachowabeba ni kuwa na wachezaji wanaojituma na wenye nidhamu ya
kupambana na kufuata maelekezo kwa muda wote wa mechi.
“Ukiwa
na timu yenye wachezaji wanaojituma na kujitambua inakuwa ni faida kwa
timu jambo ambalo linawasaidia Yanga. Hata hivyo siwaogopi, nawaheshimu
kama ninavyoziheshimu timu zote zilizo Ligi Kuu.
“Kuna
miezi sita imebaki kabla ya kuanza kwa mashindano ya Afrika kwa ngazi
ya klabu, hivyo ni mapema mno kuanza kuzungumzia mashindano hayo wakati
kuna ligi na Kombe la FA ambayo tunatakiwa kufanya vizuri.
“Hata hivyo kama nilivyosema awali kwamba mkakati wetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye kila mashindano.
“Hili litatimia tu iwapo wachezaji watakuwa na nidhamu, juhudi na malengo.”
0 comments:
Post a Comment