Waziri William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, William Lukuvi amesema mtu yoyote asiyelipa kodi ya ardhi na
kuendeleza ardhi hiyo, ni sababu tosha ya kunyang’anywa ardhi hiyo
pamoja na kufutiwa hati ya umiliki kwa kuwa anaingizia hasara serikali
Waziri Lukuvi amebainisha hayo ikiwa
imepita siku moja tokea kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Mh.
Fredrick Sumaye kudai chanzo cha kupokonywa shamba lake ni siasa tu za
yeye kuhama chama cha CCM na kwenda kuupa nguvu upinzani.
Akiongea kuhusu mashamba na viwanja
kuchukuliwa Waziri Lukuvi amesema, “Kila mtu atambue iwe ni kiwanja au
shamba kama unatabia ya kutolipa kodi ya ardhi ni sababu tosha ya wewe
kunyang’anywa shamba lako au ardhi unayomiliki.
“Imejitokeza kwa watu wachache
kuchukua ardhi kubwa kwa miaka mingi kuliko hata uwiano wa uendelezaji
wa ardhi hiyo, kwa mfano kuna hati moja hapa ambayo inapigiwa kelele
tokea mwaka 1939 imekuwa ikitembea mikono mwa watu. Sasa miaka ile watu
walikuwa wachache unapokwenda kuchukua ardhi ya kijiji hekari elfu 60
kwa mfano hivi sasa wananchi utakuwa umewaachia kitu gani?” Amesema
Lukuvi
Pia Waziri Lukuvi amesema imekuwa
kawaida ya baadhi ya watu wanapowahi maeneo huwa wanakimbilia kuchukua
sehemu zenye manufaa makubwa kwa upande wao na mwishowe wanashindwa
kuendelezaa maeneo hayo kama walivyoyakimbilia.
“Unawahi kuchukua sehemu zenye
manufaa kama mto, ardhi inayolimika, sasa unachukua hekari zote hizo
halafu huliendelezi mwishowe shamba hilo hilo tunalikuta Benki
umelikopea fedha. Kisha umepata fedha hizo unakwenda kujengea
‘apartment’ sehemu nyingine na kule wananchi wanalimezea mate.Serikali
wanatumia nguvu kubwa sana kutuliza wananchi wasivamie hilo shamba ,
halilimwi, serikali hatupati kodi”, alisisitiza Lukuvi.
Kwa upande mwingine, Waziri Lukuvi
amesema serikali imekuwa na huruma kwa miaka mingi kwa wananchi wake
lakini serikali ya uongozi huu wamekubaliana kila mtu afuate sheria
anazo paswa
0 comments:
Post a Comment