Monday, 7 August 2017

KASEKE AZIONYA SIMBA NA YANGA



Image result for kaseke

Kiungo mpya wa Singida United, Deus Kaseke amesema wapo tayari kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu na kuzionya klabu shiriki zikiwamo Simba na Yanga kujiandaa kukabiliana na ushindani mkali.
Jumamosi iliyopita, Singida ilicheza mechi ya kirafiki na Yanga na kufungwa mabao 3-2, ambapo licha ya kufungwa ilionyesha upinzani mkubwa kwa mabingwa hao wa soka nchini.
Kaseka alisema kikosi chao kimefanya maandalizi mazuri na pia kina wachezaji wazoefu ambao wana njaa ya kuwania mataji mbalimbali.
“Ligi ni ushindani na sisi tuna timu nzuri ambayo iko tayari kucheza na timu zote, kila timu imejiandaa na naona tutakuwa na msimu wenye ushindani,”alisema kiungo huyo aliyesajiliwa na Singida baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga.
Kocha Mkuu wa Singida United, Hans Pluijm alisema timu yake iko tayari kuanza Ligi Kuu na kuahidi kutoa ushindani mkubwa.
“Kuna mambo machache ambayo, katika safu ya ushambuliaji tutayafanyia kazi katika muda uliobaki ninaamini hadi kufikia Agosti 26 kila kitu kitakuwa tayari,”alisema, kocha huyo aliyewahi kuifundisha Yanga.
Singida United inayotabiriwa kutoa ushindani mkali, itaanza kampeni ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, Agosti 26 kwa kuchuana na Mwadui kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive