Simba imewatambulisha wachezaji wake wapya Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima pamoja na Mghana Nicholaus Gyan kabla ya kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Wakizungumza katika mkutano huo nahodha wa Simba, Method Mwanjali, Okwi pamoja na Niyonzima waliwashukuru wanachama wa klabu kwa kuwapokea vizuri na kuahidi kuleta mafanikio katika timu hiyo.
Afisa habari wa Simba, Haji Manara aliwatambulisha wachezaji Okwi, Niyonzima na Gyan mbele ya wanahabari.
Manara wachezaji hao watatambulishwa rasmini kwa mashabiki kesho katika tamasha Simba Day ambalo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Mazingira, January Makamba.
"Kesho tutawatambulisha rasmi wachezaji wetu wote wapya na tunategemea watacheza mechi hiyo." Siku ya kesho, Simba itacheza mechi ya kirafiki na Rayon Sports ya Rwanda wakati mchezo wa mapema utawakutanisha Simba B dhidi ya Vijana Rangers.
Kabla ya mchezo huo kuanza mechezo bora wa Ligi Kuu Bara, beki Mohamed Hussein atakabidhiwa tuzo yake.
Tuzo hiyo inatokana na kura za mashabiki wa Simba waliopiga kumchagua mchezaji bora wa msimu uliopita.
Mashabiki wa Simba wataanza kuingia uwanja wa Taifa kuanzia saa 4 asubuhi, watapata burudani za kutosha kutoka kwa wasanii mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment