Monday, 7 August 2017

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO AUGUST 8.2017 na Ally mshana

Philippe CoutinhoHaki miliki ya picha
Barcelona watawapa Liverpool pauni milioni 120 za kumsajili Philippe Coutinho, 25, baada ya Neymar, 25, kwenda Paris Saint-Germain. (Star)
Licha ya meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kusema Philippe Coutinho hauzwi, Barcelona wanazidi kuwa na uhakika wa kukamilisha usajili wiki hii kwa pauni milioni 90. (Sun)
Barcelona wanaweza kutumia fedha walizopata za mauzo ya Neymar kwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa PSG Julian Draxler, 23, ambaye wakala wake ameonekana katika mitaa ya Barcelona. (Bild)
Antonio Conte anamtaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, na pia ameitaka bodi ya Chelsea kufanya usajili zaidi baada ya kuona kikosi chake kikifungwa na Arsenal. (Daily Mirror)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp yuko tayari kuacha kumfuatilia Virgil van Dijk, na badala yake kuwaamini mabeki aliokuwa nao sasa. (Mirror)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema wachezaji zaidi wataondoka Emirates kabla ya dirisha la usajili kufungwa kwa sababu kikosi chake ni kikubwa mno. (Telegraph)
Virgil van DijkHaki miliki ya picha
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, yuko tayari kukubali hali ilivyo- ya Arsenal kugoma kumuuza- na atabakia hadi mkataba wake utakapomalizika na kuondoka bure msimu ujao. (Mirror)
Barcelona wamekubaliana na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, lakini sasa wanahitaji kukubaliana ada ya uhamisho ambayo Dortmund wamesema wanataka pauni milioni 90.2. (L'Equipe)
Barcelona wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa zamani wa Tottenham Paulinho, 29, kutoka Guanghzhou Evergrande ya China. (Sport)
Chelsea wapo tayari kupambana na Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 28, ambaye atagharimu takriban pauni milioni 90. (Express)
Chelsea, Manchester United na Monaco zinamtaka beki wa Barcelona Sergi Roberto, 25, ambaye anaweza kuuzwa kwa pauni milioni 36.1. (Don Balon)
Ousmane DembeleHaki miliki ya picha
Manchester United wamepanda dau la pauni milioni 36 kumtaka Sergi Roberto, lakini Barcelona wamesema mchezaji huyo hauzwi. (Mundo Deportivo)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameutaka utawala wa klabu yake kumsajili beki wa kulia wa Monaco, Fabinho, 23. (Don Balon)
Baada ya Nemanja Matic kwenda Manchester United kinyume na matakwa yake, meneja wa Chelsea Antonio Conte amekiri kuwa hawezi kuzuia uuzwaji wa Eden Hazard, 26, ambaye ananyatiwa na Barcelona. (Star)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza) 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive