Tuesday 8 August 2017

JAMES FOUNDATION YATIKISA KUWAFUNDA VIJANA KIUCHUMI


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya James Foundation, Leonard Manyama akizungumza kwenye Kongamanao hilo.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo
Kongamano likiendelea.
Ofisa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya ya Kinondoni, Flora Msilun akizungumza jambo.

TAASISI ya kiraia ya James Foundation leo imefanya kongamano na baadhi ya vijana wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwafahamisha fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana ndani ya Wilaya ya Kinondoni.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Sunu uliopo Tegeta jijini hapa ambapo mgeni rasmi wa kongamano hilo alikuwa Ofisa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya ya Kinondoni, Flora Msilu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurungenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Leonard Manyama, amesema vijana walioshiriki kongamano hilo vijana watanufaika na elimu waliyoipata juu ya kujikwamua kiuchumi na kukuza biashara wanazozifanya.
Amesema pia kongamano hilo linaunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kutaka kila mmoja kunufaika na rasilimali za taifa hasa kwa kufanya kazi.
Naye Flora Msilu alimpongeza mkurugenzi huyo kwa juhudi zake za kuandaa makongamano na kutoa fursa mbalimbali za kujadili juu ya kujikwamua kimaendeleo kama serikali inavyowahimiza wananchi kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo kuelekea uchumi wa viwanda.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive