Nyota wa soka wa Brazil, Neymar Jr
ametambulishwa rasmi na klabu yake mpya ya Paris Saint-Germain (PSG) ya
nchini Ufarasa baada ya kukamilisha usajili kutoka Barcelona kwa ada ya
uhamisho ya Tsh 579 bilioni ambayo imevunja rekodi ya dunia.
Wakati wa mkutano na waandishi wa
habari, Neymar alisema kwa muda mrefu alikuwa hajui hatma yake na
kwamba, wachezaji wengi wa Brazil walikuwa wakimshawishi ajiunga na PSG.
Aidha, Neymar ambaye hakueleza sababu
za kuamua kuikimbia Barcelona, amesema kwamba hajajiunga na PSG ili awe
mchezaji mkubwa klabuni hapo.
Akieleza masikitiko yake, Neymar
alisema kwamba bado anaiheshimu klabu ya Barcelona lakini amesikitishwa
na ukosoaji uliofanywa na mashabiki huku baadhi yao wakienda mbali na
kuchoma jezi zake.
Kutokana na uhamisho huo wa ghali zaidi
duniani, Neymar atalipwa mshahra baada ya makato Tsh 1.6 bilioni kwa
wiki ambapo kwa mwezi atalipwa Tsh 6.4 bilioni akiitumikia PSG.
0 comments:
Post a Comment