Kila lenye mwanzo lina mwisho, na hilo limetimia baada ya MSN kumeguka yaani neno N
kuondoka na kuacha umoja huyo ukiwa ukiwa.
Messi, Suarez na Neymar ni utatu ambao hakuna beki yoyote
duniani ambaye angependa kukutana nao, huu ni muunganiko hatari zaidi
kuwahi kuushuhudia katika ulimwengu wa soka.
Lakini sasa Suarez na Messi wamebaki wapweke baada ya muuaji mwenzao
kutua PSG kwa mkataba wa miaka 5, Messi, Suarez na Neymar walikuwa kama
ndugu chemistry iliyokuwa kati ya wanyama hawa watatu ulikuwa inatishia
sana usalama wa wapinzani.
Baada ya Neymar kuondoka Barcelona alianza Messi kwa kuandika majonzi
yake na jinsi anavyojisikia vibaya kumpoteza Neymar ambaye alikuwa kama
rafiki kwake,Neymar naye amemuandikia ujumbe Messi, Suarez na Barca
jinsi anavyojisikia kuondoka, ujumbe ambao umewaumiza zaidi mashabiki wa
Barcelona.
“Maisha ya soka yamejawa na changamoto nyingi sana ikiwemo matokeo na
nyingine za nje ya uwanja lakini Barcelona kumekuwa na changamoto
nyingi sana, nakumbuka nilifika nikiwa kijana mdogo tu mwenye miaka 21”
alianza kwa kuandika Neymar.
“Siwezi sahau siku yangu ya kwanza kufika Nou Camp na kushare chumba
na watu niliotamani kuwa kama wao akiwemo Iniesta,Puyol,Valdes bila
kumsahau Messi, hakika ilikuwa faraja kwangu kucheza Barcelona ni zaidi
ya timu”
“Najisikia faraja sana kuwahi kucheza na mchezaji bora kuwahi kumuona
na sidhani kama nitakuja kuona kama Lioneil Messi na alikuwa rafiki
yangu nje na ndani ya uwanja, yeye na Suarez walinifanya nishinde kila
kitu ambacho mchezaji anataka kushinda”
“Lakini hili ni soka na kama mwanasoka nahitaji changamoto mpya na
kwa mara ya pili ninapingana na baba yangu na kufanya ninachoona ni
sahihi na naamini utanisuport,Barcelona iko moyoni mwangu lakini
nahitaji changamoto mpya PSG”
Neymar alimalizia kwa kusema ni uamuzi mgumu alioufanya lakini kwa
umri wake wa miaka 25 anaona ni jambo sahihi na pia amefuta minong’ono
ya kwamba baba yake ndio amelazimisha usajili huo ufanyike lakini kumbe
baba yake hakutaka Neymar acheze PSG.
0 comments:
Post a Comment