Uongozi wa Yanga umetaka Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kuwaomba radhi mara moja.
Yanga
wametaka kuombwa radhi kutokana na kitendo chao cha kutoalikwa katika
zoezi la kukabidhi vifaa lililofanywa na Kampuni ya Vodacom na wao
hawakualikwa.
“Halikuwa
jambo jema na pia linatuharibia kwa kuwa jezi zetu ni mkataba wetu na
SportPesa na si Vodacom. Lakini ajabu hatukuambiwa wakati na sisi
tulikuwa tumepanga jezi hizo zifanyie uzinduzi maalum na mchezaji wa
zamani wa Arsenal, Sol Campbell ambaye anakuja nchini,” alisema Katibu
Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa.
Wakati
wa zoezi hilo, Msemaji wa Simba, Haji Manara alijitokeza kuwasaidia
Yanga kupokea jezi, jambo ambalo limechangia kuibuka kwa hasira za Yanga
ambao wameonyeshwa kukerwa na hali hiyo.
0 comments:
Post a Comment