Thursday, 3 August 2017

SINGIDA UNITED YAPATA SHAVU


Klabu ya Singida United imepata mdhamini mpya kampuni ya YARA Tanzania wameingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya zaidi ya Sh 250 milioni.
Yara ni kampuni ya Norway inayojishughulisha na masuala ya kilimo sasa watakuwa mdhamini  Singida United pamoja na Sportpesa, kampuni ya mafuta ya Puma.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusainishana mkataba huo iliyofanyika ukumbi wa hoteli ya Serena jijinj Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa YARA, Alexandre Macedo alisema wameamua kuingia Singida United baada ya kuona klabu hiyo ina nembo ya mafuta ya alizeti.
"Tunashughulika na kilimo, Singida United tuliona ni klabu inayojihusisha na kilimo cha mafuta ya kula, hivyo tumeona ni vyema kushirikiana nao maana hii ni ajira kwa vijana," alisema Macedo.
Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga aliishukuru YARA na kuahidi kushirikiana nao ikiwa ni pamoja na kuitangaza.
“Tuliomba udhamini kwao na hawakusita kwani tayari tumepata ekari zaidi ya 100 ambazo tutalima kwa kushirikiana na wadhamini wetu, pia huyu ni mdhamini mkubwa kati ya wadhamini wote tulioingia nao mkataba kwani wametoa fedha nyingi kuliko hao," alisema Sanga.
Wadhamini hao pia wametoa vifaa jezi na mipira vitakavyotumia na timu hiyo msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive