Baba mzazi wa mtoto Mwamvita Abdulilah aliyepewa msaada wa matibabu wa
Sh 2milioni na klabu ya Simba katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) ameamua kuhama kuishabikia Yanga na kujiunga miamba hiyo ya
Msimbazi.
Mwamvita aliyelazwa hospitalini hapo kwa
zaidi ya miezi miwili akisubiri upasuaji, alikuwa akisumbuliwa na tatizo
la kushindwa kupumua vizuri kutokana na kuwa na tundu kwenye moyo
amepona na anatarajia kuruhusiwa muda wowote kuanzia sasa.
Baba
mzazi wa mtoto huyo, Abdulilah Bakari alisema amehangaika na mtoto huyo
kwa takribani miaka mitatu na hivi sasa nashukuru Mungu kwani amepona
baada ya kupatiwa matibabu.
"Nashukuru sana kwa dhati
Simba, mimi nilikuwa Yanga damu damu, lakini kutokana na kile ambacho
Simba wamenifanyia kutoa Sh2 milioni kumtibia mwanangu nimehama rasmi na
sasa nimehamia Simba mimi na familia yangu," alisema Abdulilah.
Naye
mtoto Mwamvita alisema anashukuru wanasimba wote kwa kujitoa kuokoa
maisha yake, "sasa nitaweza kurudi masomoni nashukuru kwa nafasi hii
waliyonipa naomba Mungu awaongezee walipopunguza."
Akizungumza
MCL Digital leo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi
alisema baada ya kupatiwa fedha hizo za matibabu, walimfanyia upasuaji
Mwamvita Agosti 24 mwaka huu.
Alisema upasuaji huo
ulifuatia baada ya viongozi na wachezaji wa Simba kutembelea taasisi
hiyo Agosti 7 mwaka huu katika maadhimisho ya Simba Day na kukutana na
Mwamvita ambaye alikuwa akisubiri kufanyiwa upasuaji.
"Walikuja
kutoa msaada kwa watoto wenye matatizo ya moyo na ndipo walipokutana na
Mwamvita na kutoa msaada huo, tunashkuru sana kwa msaada huu na
tunakaribisha klabu nyingine kutoa msaada pamoja na TFF ili watoto wengi
zaidi wasaidiwe," alisema.
Alielezea kuhusu afya ya
Mwamvita, Profesa Janabi alisema kwa sasa anaendelea vizuri na
ameshapona tatizo linalomsumbua baada ya kufanyiwa upasuaji.
"Tulimfanyia
upasuaji mkubwa wa kufungua kifua, amepona na tunatarajia kumruhusu
kurudi nyumbani wakati wowote kuanzia sasa," alisema.
CHANZO MWANASPOT
0 comments:
Post a Comment